Wema Isaac Sepetu.
Habari za uhakika zilizopenyezwa kwenye gazeti hili zilieleza kuwa, Wema yupo tayari kwa lolote juu ya hukumu hiyo.Katika kesi hiyo ya Wema iliyokuwa ikiunguruma katika Mahakama ya Mwanzo Kawe jijini Dar tangu Agosti mwaka huu alipotenda kosa hilo, Wema amekuwa akisali usiku na mchana tangu alipojulishwa kwamba hukumu yake itakuwa Jumatatu ya Novemba 25.
Habari zilieleza kuwa Wema aliungana na mwenzake, Masanja Kajala katika kufunga kwa maombi kwa kuwa kesi zao zitatolewa hukumu kwa siku moja (Jumatatu ijayo).
Gazeti hili lilimtafuta Wema ili kusikia ana lipi la kusema juu ya hukumu hiyo lakini hakupatikana, badala yake, meneja wake, Martin Kadinda alikuwa na haya ya kusema:
“Wema yupo tayari kwa hukumu. Amejipanga vizuri kwa kazi zake. Anaamini kabisa hukumu itakayotolewa na hakimu ni mipango ya Mungu.
“Lakini pamoja na hayo aachi kusali au kuomba dua ili Mungu amtendee muujiza katika hukumu hiyo.”
Tofauti na Wema, Kajala yeye hukumu yake itahusu ile kesi ya kutakatisha fedha haramu akiwa na mumewe, Faraji Chambo.
Mwaka 2009, Wema alidakwa na Polisi Kituo cha Magomeni, Dar na baadaye kupandishwa katika Mahakama ya Kinondoni kwa
Hakimu Emilius Mchalu kwa kosa la kuvunja kioo cha gari la aliyekuwa staa wa filamu za Kibongo, marehemu Steven Kanumba.
Hata hivyo, Kanumba aliamua kuifuta kesi hiyo kwa sababu ya kutaka amani. Wakati huo Wema alikuwa na uhusiano wa kimapenzi na mjasiriamali aitwaye Jumbe Yusuf Jumbe.
Kama vile haitoshi, mwaka 2011, Wema huyohuyo alilikwaa soo jipya, akakamatwa na Polisi wa Kituo cha Oysterbay na kufikishwa Mahakama ya Mwanzo, Kinondoni kwa kosa la kumtusi na kumtishia maisha mwanamuziki wa Bongo Fleva, Raheem Rumy Nanji ‘Bob Junior’.
Katika hukumu ya kesi hiyo Wema alilipa faini ya shilingi elfu arobaini badala ya kifungo cha miezi sita jela hivyo hiyo itakuwa hukumu nyingine inayosubiriwa kwa shauku kubwa na mashabiki wake.
No comments:
Post a Comment