Social Icons

Dondosa Twitter Facebook

Thursday, November 14, 2013

AIBU KUBWA..!MBUNGE "PRO. JUMA KAPUYA" NDIYE ALIYEMBAKA MWANAFUNZI WA MIAKA 16 NA KUMUAMBUKIZA VVU NA KUMTISHIA KUMUUA

Kulia ni MH. PROF JUMA KAPUYA (MB) akiwa na msanii DOKII
MBUNGE wa Urambo Magharibi, Profesa Juma Kapuya (CCM), ameingia katika matata. Katika kujaribu kudhibiti mtoto wa shule ambaye anadai alibakwa naye na kuambukizwa virusi vya ukimwi, mbunge huyo ametoa vitisho vya kuua mtoto huyo na kujiua kama njia ya kuepuka dhahama inayoelekea kumkabili.

Siku moja baada ya gazeti  la  Tanzania Daima  kuripoti habari za mbunge mmoja (bila kumtaja jina), jana asubuhi Profesa Kapuya ameibuka na kumtisha mwanafunzi huyo mwenye miaka 16 anayesoma Shule ya Sekondari Turiani iliyoko Magomeni jijini Dar es Salaam.

Baada ya kujua kuwa mtoto huyo ndiye alitoa habari za masahibu hayo, ambayo mbunge hakutaka yajulikane, alimpigia simu mtoto huyo, na baadaye kutuma meseji kadhaa za vitisho.

Jana Tanzania Daima ilishuhudia baadhi ya meseji za simu zilizotumwa na Profesa Kapuya kwenda kwa mtoto huyo.

Alfajiri saa 11:21 kupitia simu yake ya mkononi yenye namba 0784993***, Profesa Kapuya alituma ujumbe ufuatao kwa mtoto huyo: “chagueni kunisubiri tuje tuongee au mnataka kufa?” 

Baadaye saa 1:07 asubuhi, alituma ujumbe mwingine kutoka simu hiyo hiyo kwenda kwa mtoto huyo, ukisema: “Mkiuawa, itakuwa nzuri, itawapunguzia gharama za kuishi. Usitake kugombana na serikali, mtoto mdogo kama wewe. Sisi ndo wenye nchi yetu.

“Mwambieni Mbowe mwenye hilo gazeti awape nyumba ya kuishi. Si mmemuingizia hela leo? Mnatumika bure watu wanaingiza hela nyingi, mmenitibua lazima niwauwe wiki hiii haitaisha, nitapanga kambi popote.

“Jana si wamekuficha? Tuone kama utalindwa milele. Kazi ya kulindwa imeisha, maana wameshatengeneza hela. Lazima mvae sanda. Hilo sio ombi, ni wajibu wenu. Mnajitia mafia watoto sio? Watoto wetu wanauza unga, nani anawakamata? Nani atapigana nasi?” 

Hata hivyo, baada ya kuhisi kuwa watoto hao wamedhamiria kumchukulia hatua, na wamewasiliana na taasisi mbalimbali za kiraia na serikali zenye uwezo wa kumtia adabu, mbunge huyo alimtumia mtoto huyo ujumbe wa kuonyesha alikuwa anafikiria kunywa sumu.

No comments:

Post a Comment