MR BLUE |
Hitmaker wa ‘Mapozi’ Mr. Blue aka Kabayser anatafutwa na polisi wa
Kenya. Msanii huyo anatafutwa kwa shutuma za kushindwa kutokea kwenye
show aliyokuwa amesaini mkataba huko Mombasa, Kenya. Mr. Blue alikuwa
anatakiwa kutumbuiza kwenye maeneo ya Office Restaurant, Likoni na
Mariakani Jubilant Hotel, November 16 na 17.
Mratibu wa show hiyo, Sammy Ondwar Onyango, aliamua kwenda kushtaki
polisi sababu anadai alikuwa ameshamlipa msanii huyo sehemu ya malipo
waliyokuwa wamekubaliana.
“Mr Blue si mtu mwaminifu kabisa. Aliwahi kuniangusha pia mwaka 2012
kwenye show ya Jet Bar, Likoni, baada ya kudai kuwa alikosa basi ya
kwenda Mombasa na nililazimika kuingia zaidi mfukoni kumlipia basi
jingine,” Onyango aliliambia gazeti la The Star.
Promota huyo amesema kwenye tukio la sasa, walikubaliana kumlipa
shilingi 100,000 (za Kenya) ambazo ni sawa na shilingi milioni 1.8 na
tayari alikuwa ameshamlipa shilingi 40,000 kupitia M-Pesa.
Kesi hiyo imeripotiwa kwenye kituo cha polisi cha Likoni.
Gazeti hilo limesema baada ya kuwasiliana na Mr Blue kwa simu, aliweza
kujibu kwa ujumbe mfupi wa simu kwamba alikuwa akiendesha gari na simu
haikupatikana tena.
No comments:
Post a Comment