Msanii wa muziki wa kizazi kipya na mwenye tuzo kibao za kimataifa Ambwene Yesaya AY.
Wajumbe wapya wa Bodi ya Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA), wametaka kupewa miezi sita, wasanii waanze kufaidi matunda yao.
Akizungumza
kwa niaba ya wajumbe wenzake wa bodi hiyo iliyozinduliwa juzi, Alex
Msama alisema Basata kuna changamoto nyingi ikiwemo kukosa vyanzo vya
kutosha vya mapato hivyo changamoto kubwa iliyopo mbele yao ni
kuhakikisha Basata inajiendesha yenyewe.
“Tutaboresha
kazi za wasanii kwa kuziinua na kuzilinda kwa nguvu zote, tutasimamia
studio zitoe kazi bora za wasanii sio bora kazi, tunataka ifike mwisho
wasanii kwenda kurekodi Afrika Kusini, China na kwingineko na kazi zetu
zivuke mipaka.
“Ndani
ya miezi sita, matunda yetu yataanza kuonekana, kikubwa tunaomba
ushirikiano kwa wasanii na wadau wote wa Sanaa.”alisema Msama.
Naye
Mwenyekiti wa Bodi ya Basata, Profesa Penina Mlama alisema
anasikitishwa na vitendo vya mmomonyoko wa maadili unaofanywa na wasanii
ambao ni kioo cha jamii na badala yake wamekuwa ni wachafunzi wa
maadili.
“Kuna
umuhimu wa kuendesha kampeni ya kitaifa nchi nzima kupinga ubomoaji wa
maadili na kuelimisha wasanii pamoja na hadhira yao na watanzania kwa
ujumla kuhusu umuhimu wa sanaa katika kujenga maadili ya taifa.
No comments:
Post a Comment