skip to main |
skip to sidebar
AJIRA KUTOKA KWA RAY C..!! MTU WA KUFANYA KAZI HII NDIYO ANAHITAJIKA KUTOKA KWA RAY C
Umem-miss yule ‘Kiuno Bila Mfupa’ wa enzi hizo? Vumilia kidogo kwa
sababu yuko mbioni kurudisha ile figure yake. Mwimbaji wa ‘Uko Wapi’,
Rehema Chalamila aka Ray C amesema ameli-miss umbo lake la mvuto
alilokuwa nalo zamani alipokuwa mwembamba kiasi, wataalamu wa lugha
nyepesi wanaita ‘Kipotabo’.
Hali hiyo imemfanya
Ray C kutangaza ajira ya kumtafuta Personal Trainer atakayemsaidia
kumrudisha enzi zake. Kupitia Instagram, Ray C amepost picha inayoonesha
umbo lake la zamani akiwa anatumbuiza na kuandika, “I miss ths sexy
body!!!!Heeeeelp....I need a good trainer........!Whr r U!!!!!!” Hii ni
nafasi ya ajira, kama we ni mtaalam wa mambo hayo mtafute Ray C.
No comments:
Post a Comment