Social Icons

Dondosa Twitter Facebook

Saturday, November 30, 2013

Hii Ndio Video Inayomponda Diamond,Mdogo Wake Aiachia Hewani[Video]


Huyu Ndiye Mwanamke Aliyepigwa Na TID Na Kusekwa Rumande,Kisa Mapenzi Na Wivu[Picha]



Msanii mahiri wa muziki wa kizazi kipya, Khaleed Mohamed 'TID' yupo mahabusu katika Kituo cha Polisi Oysterbay tangu jana usiku baada ya kukamatwa na polisi kwa tuhuma za kumpiga na kumjeruhi msichana anayedaiwa kuwa ni mpenzi wake,  Mariam Nnauye.
 Huyu Ndio Mariam Nnauye. Taarifa zinasema kuwa ugomvi ulianza maisha club jana usiku baada ya TID kumkuta Mpenzi wake akiongea na mwanaume mwingine bila ruhusa ya Top In Dar na ndio Top akamvuta mpenzi wake na kumpiga makofi.Bila kujali mapenzi yao binti huyo alikwenda moja kwa moja kituo cha polisi Oysterbay na kutoa taarifa ya kupigwa na Tid.

Tid ametoka mida ya saa tano asubuhi kwa Dhamana na ataripoti tena polisi jumatatu.

Baby Madaha-'Diamond Si Msanii,Ni Mpenda Ngono'

MSANII filamu na muziki wa kizazi kipya wa Tanzania Baby Joseph Madaha maarufu kwa jina la (Baby Madaha) amesema kwamba msanii mwenzake wa muziki nchini,Naseeb Abdul maarufu kwa jina la Diamond Platinumz si msanii bali ni mfanyabiashara. 
Madaha amesema kwamba Diamond si mwanamuziki na kwamwe huwezi kumlinganisha na msanii kama Barnaba Boy, anayefanya muziki kama sanaa na kazi kulingana na kipaji chake na kwamba Diamond si msanii wa muziki bali ni msanii ngono anayefanya biashara ya muziki kupitia mapenzi.

Baby madaha ambaye hivi sasa yuko nchini Kenya kwa shuguli za muziki amesema kwamba, Diamond hajui kuimba na ndiyo maana amekuwa msanii wa matukio huku nyota yake ikiegemea kwenye mapenzi na wasichana wenye majina makubwa hususn wasanii.
Akizungumza na kandili yetu katika mahojiano maalum leo baby Madaha alisema kwamba, "Binafsi niliposikia kwamba Diamond anaumiza kichwa kunasa penzi la msanii Elizabeth Michael maarufu kwa jina la (Lulu) sikushangaa hata kidogo. kwa sababu nilitambua kwamba soko lake la muziki limeanza kushuka hivyo lazima atafute eneo lingine la kujiimarisha kibiashara, ili jina lake liendelee kuwika". 

"Siku wanawake maarufu nchini Tanzania watakapo jitambua na kuacha kulewa penzi la Diamond ndiyo itakayokuwa mwisho wa maisha yake kimuziki,kwa sababu hatakuwa na jipya na hivyo soko lake litaanza kuporomoka"alifafanua Baby Madaha. 

Thursday, November 28, 2013

HUYU NDIYE MSANII PEKEE WA BONGO AMBAYE BARACK OBAMA AMEM-FOLLOW KWENYE TWITTER...!! BOFYA HAPA KUMJUA.

obby

Hii itakuwa ni kwa mara kwanza kwa mwimbaji wa Tanzania na pengine Afrika kuwa followed na Rais Barack Obama wa Marekani kwenye twitter ambae ana zaidi ya followers milioni 40 lakini yeye anafollow watu laki sita.

Vanessa Mdee ameingia kwenye list ya watu laki sita ambao Rais Barrack Obama ana wa-follow sasa hivi ambapo baada ya Rais huyu kufollow, kwa furaha Vanessa alishare kwenye instagram screenshot ya ukurasa wake wa twitter ukionyesha Barack Obama ameanza kum-follow.

Kama ilivyo twitter, hii inamaanisha ana Vanessa ana uwezo wa kumuandikia msg binafsi kwenye inbox Rais Obama.

vanesaobama
vmoney
vn



PREZZO Ametisha Baada Ya Kuonyesha Bunduki Yake Ya Dhahabu

Msanii anayekumbwa na tetesi ya kuwa amekuwa maskini Mr. President aka Prezzo, ameamua kuonyesha kuwa yeye bado ni mmiliki wa game ya hip-hop nchini Kenya.
Hivi maajuzi msanii huyu anayekisiwa kuwa ni miongoni mwa wasanii tajiri Kenya alikuwa akirushiana matusi na msanii Huddah Monroe baada ya wawili hao kuachana.

Katika mtandao wake wa Instagram, Prezzo kando na kuwaonyesha kuwa yeye ana pesa na hana time ya kujihusisha na madada wakware, aliwatisha wasanii na mahasimu wake kwa kuwaonyesha bunduki yake iliyotengenezwa kwa dhahabu.

Uvumi wa kuwa yeye ameishiwa kifedha utabaki kuwa uvumi kwani Prezzo anaendelea kuogelea ndani ya dhahabu na kuishi maisha kama ya 'president'

KWANINI BAADHI YA WATU WANACHUKIA MAFANIKIO YA DIAMOND? ...TATIZO NI ‘BEI YA MKAA’....SOMA ZAIDI HAPA

Watu wengine kamwe hawataweza kukusifu au kukubali kwa unachokifanya mpaka pale usipokuwepo kabisa.. Ni ajabu kuwa watu wengine katu hawawezi kuona kile walichonacho; wakionacho pekee ni kile wasichonacho, ni kile wanachokosa. 


Wakati mwingine inahitaji roho ya paka kuendelea na nguvu kufanya kile unachofanya wakati watu wanaendelea kukudhihaki.

Zaidi ya muziki, kuna kitu gani kizuri kinachoitangaza Tanzania nje ya nchi kwa sasa? Tusaidiane kuuchambua ukweli huu unaomezeka kwa fundo la mate la kulazimisha kinywani.
 

Ni lini mara ya mwisho Tanzania imefanya vizuri kimataifa kwenye soka? Hakuna habari njema zaidi ya kuendelea kuwa kichwa cha mwendawazimu, iwe kwetu hata nje

Ni lini mara ya mwisho mkimbiaji riadha wa Tanzania ameshinda mbio zozote za kimataifa? Hakuna. 

Kimichezo ni kama bado tumeendelea kuwa wasindikizaji tu. Au umesahau jinsi Selemani Kidunda alivyodundwa mwaka 2012 kwenye mashindano ya Olimpiki? Ukitoa mwaka 2005 pale Nancy Sumari alipokuwa Miss World Afrika, ni lini mrembo yeyote wa Tanzania amewahi kuiletea sifa nchi yetu? 

Ni nini hasa kinachoweza kuifanya Tanzania kuipeperusha bendera yake kwenye jukwaa la kimataifa kwa sifa nzuri? Au labda kipindi hiki tumegeuka kuwa mabingwa wa biashara ya dawa za kulevya na Watanzania ndio wamekuwa vinara wa kukamatwa kila kukicha nchi za nje.

Angekuwepo Kanumba na zile jitihada alizokuwa akizifanya, labda tungesema Bongo Movies ilikuwa inaelekea kuwa njia nzuri ya kutupa heshima pia. Lakini tangu afariki, hakuna mwingine anayeonesha dalili za kufanya kile alichokuwa anakifanya na filamu zetu zimeendelea kuwa za nyumbani pekee.

Hivyo, ukiangalia kwa mifano hiyo, ni muziki pekee wenye matumaini ya kuliongezea ‘kiki’ jina la nchi yetu kwenye ‘google search’. Lakini kama muziki ndio unaonekana kuwa kitu muhimu kinachoitangaza Tanzania, mbona wale wanaofanya vizuri kwa kutuwakilisha nje tunawabeza?

Mpaka muda huu, ukimtoa AY, hakuna msanii mwingine wa Tanzania anayevuma kimataifa kama alivyo Diamond Platnumz. Amefanikiwa kiasi cha hivi karibuni kumshirikisha staa wa Nigeria Davido kwenye remix ya wimbo wake, Number 1 na video iliyogharimu si chini ya dola 25,000 iko mbioni kutoka. Amekuwa ni msanii mwenye kujituma, kutake risk na kutochoka kujaribu kufanya kile wengi wamekuwa wakikiogopa kufanya. Lakini bado kuna watu wengi hawaoni anachokifanya na wameendelea kumkejeli.

Wanasema hakuna binadamu aliye mkamilifu, lakini pamoja na kwamba unaweza kumnyonga mnyonge, ni vyema kukumbuka kumpa haki yake. Ni asili ya mwanadamu kuumizwa na mafanikio ya mtu mwingine, na ndio kinachotokea kwa Diamond. Ameendelea kufanikiwa kiasi mpaka anaanza kuwakera wengine. Si kosa kuchukia maisha na scandal zake, lakini si kosa pia kusifia kile anachoifanyia Tanzania.

Siwezi kubisha kuwa, mimi binafsi Diamond amekuwa akinikera kwa baadhi ya vitu (kama mimi pia ninavyokera wakati mwingine, nobody is perfect) lakini siwezi kuukataa ukweli kwamba Diamond ana kipaji, anajituma, anapendwa na anajua anachokifanya. Kubwa zaidi ya hayo, Diamond amekuwa mstari wa mbele kuitangaza Tanzania na Kiswahili pia lugha yetu adhimu kupitia nyimbo yake.

Ni jambo tunalolihitaji Watanzania kuwa na msanii wetu mkubwa mwenye hadhi na mafanikio kama ya P-Square. Pengine tusisahau ukweli huu kwamba ni mapenzi watakayoyapata wasanii wetu hapa nyumbani pekee ndio yatakayowapata mafanikio zaidi. Utafanikiwa vipi nje ya nchi kama nyumbani wanahate?

P-Square walikiri kuwa ni Wanaijeria wenyewe ndio waliowafanya wawe wakubwa kiasi hicho na kuwataka Watanzania pia wafanye hivyo kwa wasanii wao.

“Wanamuziki wenu wanafanya kile kile sisi tunachokifanya, mnaowaona watu hawa hapa?Mnaweza kuwafanya wawe wakubwa kuliko P-Square. Ukweli ni kwamba tunapromote muziki wa Africa. Waafrika huu ni muda wetu. Wamarekani nasema wanaogopa sasa hivi. 

Ningependa kuona mnaweka jitihada zaidi kwa wanamuziki wenu hapa. Nataka kuwaona wanakuja Nigeria na kuongoza concert. Hakuna mtu anayeza kufanya hivyo vizuri isipokuwa ninyi,” alisema Peter kwenye mkutano na waandishi wa habari jijini Dar, siku moja kabla ya show yao ya Leaders Club.

Diamond ni binadamu kama wengine. Anaumia anapoona anakosolewa hata katika mambo yasiyokuwa ya msingi. Kwa mfano hivi karibuni alihudhuria harusi ya Peter wa P-Square jijini Lagos, Nigeria. Inasemekana kuwa mwaliko huo aliupata kutokana na kuwa karibu na Iyanya aliyemshirikisha kwenye wimbo wake. Katika harusi hiyo, Diamond alipiga picha na Peter na kuiweka Instagram.

Diamond akiwa na Peter Okoye
Inasemekana kuwa P-Square walipokuja Tanzania waliulizwa kama wanamfahamu Diamond na kwamba wakasema lahashaa, hawamjui. Cha ajabu suala hilo limegeuka gumzo na watu wamekuwa wakimkejeli Diamond kuwa kaumbuka. Jamani, kwani ni lazima Peter awe anamfahamu Diamond? 

Amfahamu kwa njia ipi? P-Square ni wasanii namba moja Afrika, unaweza kufikiria ni wasanii wangapi Afrika wenye level za Diamond wanaotaka walau kupata contacts zao? Ni wengi mno, na unadhani ni rahisi kuwapata? Na hata hivyo, wote tunajua harusi zinavyokuwa na pilikapilika, unahisi Peter alikuwa na uwezo wa kumkariri kila mtu aliyehudhuria harusi yake. Unadhani ilikuwa rahisi kwa Diamond kujitambulisha vizuri kwa Peter kiasi cha kumfanya amkumbuke? Ni ngumu.


Haya, jana Rais Jakaya Kikwete alisema kwenye semina ya fursa kuwa Diamond ni msanii mwenye nidhamu ya kazi ama kwa Kiingereza ni ‘work ethic’. Wengi wemepingana na kauli ya mkuu wa nchi kwa kuona kampa Diamond sifa asiyostahili.

Lakini kwanza tujiulize, ni nini maana na nidhamu ya kazi? Ni thamani iendanayo na uchapakazi, umakini na kujituma. Nidhamu ya kazi ni pamoja na kuwa ‘reliable’ kuwa na uwezo wa kuanzisha vitu na kutafuta ujuzi mpya. Kwa tafsiri hiyo, unaweza kumpiga Rais Kikwete kwa kusema Diamond ana nidhamu ya kazi? Maisha binafsi, scandal na ubinadamu, havina uhusiano wowote na nidhamu ya kazi. 



Sibishi kuwa wakati mwingine maisha ya Diamond hasa ya kimapenzi yamekuwa na sifa mbaya, lakini hiyo haiuondoi ukweli kuwa, ni msanii anayejituma sana. Tumkosoe pale ambapo anastahili kukosolewa na pia tumpe sifa pale anapostahili kusifiwa lakini sio kuhate pasipo na sababu za msingi.

Labda wengine wanamchukia kwasababu hupenda ‘kubrag’ kwa kupost picha za dola, cheni, saa, nguo ama viatu vya thamani kwenye Instagram? Kama ndivyo, basi nakumbuka kauli ya Joh Makini aliyoniambia hivi karibuni kuwa watu wengine wamekuwa na chuki kwa wenzao waliofanikiwa kwakuwa maisha kwao ni magumu.


“Ukichungumza kitu gani kinachosababisha haya mambo yote, utagundua kuwa watu wengi hawawezi kukidhi gharama za maisha jinsi ambavyo zinapanda. Huo ni mwanzo wa kuwekeana chuki kwenye kazi au mtu anakuwa anakusikia wewe kwa kitu ambacho unafanya, utagundua ni kwamba kwasababu yeye anashindwa kulipia bili zake za kila siku, hata kama hausikika kwa namna moja au nyingine kwenye kipato chake lakini unakuta tu mtu anakuwa na chuki binafsi. Tatizo bei ya mkaa,” alisema Joh.

Ina make sense hata hivyo. Unapogundua kuwa huduma ya maji imekatwa nyumbani na huna hela ya kulipa au mchana unapita mkavu bila ‘kupiga menu’ halafu kwenye Instagram unaona picha ya Diamond akiwa na buruguntu la dola za kimarekani, lazima kiroho kiume na unajikuta unageuka hater ghafla!!!

Tatizo ni bei ya Mkaa.

EXCLUSIVE: SIRI 5 ZA WOLPER ZAVUJA ..Soma zaidi hapa

Wolper akifunguka ndani ya Ofisi za Global Publishers, Bamaga-Mwenge jijini Dar.
MOYO huhifadhi mengi mazito hasa ya kuumiza! Staa mkubwa wa sinema za Kibongo, Jacqueline Wolper Massawe amejikuta akimwaga machozi wakati akianika siri tano nzito kuhusu mapenzi katika mahojiano (exclusive interview) na Amani kwa takriban saa mbili.

Katika ‘intavyu’ hiyo iliyofanyika Jumatatu iliyopita kwenye Ofisi za Global Publishers, Bamaga-Mwenge jijini Dar kuanzia saa 8:44 alasiri hadi saa 10:44 jioni, Wolper alifunguka vitu vingi.

KISA/MKASA
Akizungumza kwa masikitiko, uchungu na majuto, Wolper alisema hawezi kumsahau mwanaume huyo ambaye ni Abdallah Mtoro ‘Dallas’ kwa namna alivyomwingia kijanja na kutaka kumvunjia heshima aliyoijenga karibia miaka kumi nyuma.
Wolper akijibu maswali ya Global.
ALIANZIA WAPI NA DALLAS?
“Siku ya kwanza Dallas alinipigia simu na kuniambia aliniona Magomeni (Dar). Naikumbuka sana siku hiyo, ilikuwa baada ya mizunguko yangu, mwanzoni sikupokea simu yake kwa sababu ilikuwa namba ngeni kwangu.


“Nilimsikiliza sana. Jamani yule mwanaume anaongea kwa ushawishi wa hali ya juu mno. Nilishangaa aliponieleza kila kitu kuhusu familia yangu na nyumbani kwetu. Kumbe tayari alishaunda urafiki na baba yangu (mzee Massawe).

“Mwanzoni nilidhani ni tapeli. Nikamkatia simu. Akaendelea kunipigia na nilipoona imekuwa kero kubwa nilipokea. Ili kuthibitisha anawajua wazazi wangu, alinitajia namba zao za simu ambazo ni za kweli.

“Pamoja na hilo nilimfanyia nyodo, si unajua mtoto wa kike? Lakini aliniongelesha kwa upole hadi nikapunguza nyodo zangu.

“Aliniuliza nataka anifungulie biashara gani. Nikamwambia biashara ya nguo. Akaniuliza nataka mtaji kiasi gani. nikamwambia dola laki moja kwa sababu nilikuwa sitaki fremu moja, nilitaka nyumba nzima. Akaniambia hakuna tatizo.

“Pia aliniuliza naishi wapi? Nikamwambia Sinza (Dar) alionesha dharau kwenye simu akaniambia atanihamishia Mbezi Beach.

“Aliniuliza natembelea gari gani? Nikamwambia Toyota Noah. Akaniambia ningependa aninunulie gari gani? Nikamjibu Toyota Discovery lakini yeye akasema ataninunulia Toyota Harrier.

“Kweli baada ya siku mbili-tatu nililetewa Toyota Harrier nyeusi nyumbani. Niliogopa isijekuwa mtego nikaingia kwenye matatizo hivyo nilimzungusha mtu aliyeniletea hadi Sinza-Mori nikamwambia apaki kwenye kituo cha teksi, nikaenda na dereva nikalichukua hadharani ili lolote likitokea nipate msaada.

“Nilikabidhiwa funguo za lile gari na documents zake, nikaondoka nalo hadi nyumbani kwangu. Kesho yake Dallas alimtuma mtu aniletee dola za Kimarekani 15,000 (zaidi ya Sh. milioni 24). Nilipouliza za nini aliniambia ni kwa ajili ya shopping ya kutembelea Harrier niachane na zile swaga za kwenye Noah (fedha inaongea). Kisha akanitumia cheni ya dhahabu.

“Siku iliyofuata alinitumia Sh. milioni 15 nipeleke nyumbani nikawaambie wazazi nimepata mchumba ambaye angeenda kujitambulisha baadaye. Niliwaambia ni Dallas ambaye walikiri kumfahamu kwa sababu alishawapigia simu na kujitambulisha kuwa ni mkwe wao.”

AMESHAKUTANA NA DALLAS?
“Hadi hapo nilikuwa sijamuona Dallas kwa sura na fedha nilikuwa natumiwa kila siku.
“Wakati hayo yakiendelea akaagiza nihamishiwe Mbezi Beach na kununuliwa lile gari lililoibua mzozo BMW X6.

“Nakumbuka siku niliyokabidhiwa lile gari nililia sana. Sikuamini macho yangu kwa sababu Dallas aliniambia amenitumia kazawadi kumbe ni BMW X6 (lina stori ndefu inakuja)!

“Kumbuka mwanzoni nilikuwa na boyfriend ambaye tulipendana sana lakini hatukupanga kufunga ndoa. Nilimweleza kila kitu akakubaliana na mimi japokuwa aliumia.
“Maskini! Kuanzia hapo nikawa nimeachana na yule boyfriend wangu lakini hakukuwa na namna kwa sababu niliamini nimepata mchumba wa kunioa.

ATAKIWA KUBADILI DINI
“Baadaye Dallas aliniambia nimeshakuwa mchumba wake hivyo nibadili dini. Kweli nilibadili nikawa Muislam na jina langu likawa Ilham. Hicho kilikuwa kipindi kigumu sana maishani mwangu kwa sababu nilionekana ni muasi katika dini yangu ambayo mama ni mzee wa usharika na mwimba kwaya, baba ni mtu wa kanisani sana.”

NINI KILIFUATA?
“Siku moja nilikuwa Tanga nashuti filamu, nilikuwa nikitoka hapo niende Morogoro. Dallas alinipigia simu akaniambia yupo Nairobi (Kenya) anakuja Tanzania. Nilimwambia nipo Tanga akaniambia atanifuata kule. “Niliendelea kupiga mzigo. Zilipita saa nyingi, baadaye nikiwa na kruu yangu, Dallas alinipigia simu akaniambia ameniona.
“Nilikataa, akaniambia namna nilivyo, nguo nilizovaa na watu niliokuwa nao, alipatia. Kumbe alikuja na Toyota Prado.

WOLPER MORO, DALLAS DAR
“Tulipomaliza kurekodi Tanga tulikwenda Morogoro, yeye aliniambia anaelekea Dar. Tulikuwa tunawasiliana. Nilipomaliza kurekodi Moro nilirejea Dar. Hapo ndipo vituko vikawa juu ya vituko.

“Niliambiwa mara kaonekana sehemu akiwa na mwanamke au wanawake. Mimi sikujali kwa sababu nilipomuuliza aliniambia hatuwezi kuonana kwa sababu kipindi hicho alikuwa katika swaumu hivyo akionana na mimi nitamharibia. (ulikuwa mwezi mtukufu).

BADO HAWAJAKUTANA?
“(Mguno) Hapo bado hatujakutana lakini yupo mjini na amejaa tele kwenye kumbi za starehe.

“Baada ya kumaliza swaumu, siku moja aliniambia anakuja nyumbani Mbezi Beach. Niliwaalika marafiki zangu tukapika vyakula, tukafanya usafi na kufukiza udi chumbani. Nilitandika mashuka meupe kitandani na kujipara kisha nikavaa ushungi kuanzia mchana nikakaa kama malkia nikimsubiri mchumba.

“Huwezi amini, hadi giza linaingia Dallas hakutia mguu. Nilipataje aibu kwa rafiki zangu waliotaka kumuona huyo mchumba? Ninyi acheni tu!
“Nilipomuuliza aliniambia alipata dharura kuna biashara alikuwa anafanya

HATIMAYE WAKUTANA LAKINI…
“Nilikasirika sana, nikasema huyu ni mchumba gani asiyetaka kuja kwangu? Nikampa muda wa siku tatu aje nyumbani na alete nguo zake zote. Kweli, siku ya tatu,  asubuhi nilimsikia mtu akiita ‘Ilham Wolper Dallas’. Nilishajua sauti yake kupitia simu hivyo nilimkaribisha na nguo zake nikaingiza ndani. Lakini cha kushangaza alikuja na pikipiki!

“Alishinda nyumbani siku hiyo maana kuna ndugu zake walikuja. Hatukufanya chochote. Dallas aliishia kunibusu shavuni kisha jioni akaondoka.

“Mjini kukawa hakukaliki. Natumiwa picha akiwa na wanawake tofautitofauti. Mmoja wa wanawake hao niliambiwa eti ana ‘ngoma’! Jamani hii dunia ina kichaa!

“Muda ukasonga, vitimbi vikawa vingi. Dallas simuoni. Muda wa kukaa kwenye ile nyumba uliisha hivyo nikahama na nikamwambia akachukue nguo zake.

UCHUMBA WAVUNJIKA, SASA ANAPUMZIKA HAPA
“Baadaye uchumba ukavunjika tena mimi ndiyo nilimwambia simtaki tena. Nilikaa muda hadi baadaye nilipopata mwanaume wangu wa sasa. Anani-control vizuri kwa sababu kanipita umri na ana busara. Tunapendana sana. Najuta kumfahamu Dallas. Siwezi kusahau tukio hilo katika maisha yangu. Dallas alicheza na hisia za moyo wangu. (akaangua kilio) Niliteseka sana. Ni Mungu tu anajua…

VIPI KURUDIA UKRISTO?
“Nimekaa muda siendi kanisani. Nilikuwa najifungia ndani nalia kama mama yangu alivyokuwa anafanya. Siku moja nilimwambia mwanaume wangu akaniambia kuliko kulia kila siku bora nirudi kanisani. Ndipo nikarudia ukristo. Kwa sasa nasali Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT), Usharika wa Kijitonyama, Dar,” alisema.

MBALI NA DALLAS
Kwa mara ya kwanza Wolper alikubali kuorodhesha listi ya wanaume aliowahi kuwa nao kimapenzi kwa kuwachambua mmoja mmoja.

ALI KIBA
Bila kupepesa macho, Wolper alikiri kuwa msanii wa Bongo Fleva, Ali Saleh Kiba ndiye aliyemfundisha mapenzi: “Ni kitambo kidogo. Wote hatukuwa mastaa lakini yeye alifanikiwa kuchomoka. Kabla ya Ali (Kiba) nilikuwa na mwanaume lakini hatukuduu kwa maana ya utu uzima, ilikuwa yale ya kitoto. Lakini Ali ndiye hasa aliyeniingiza kwenye ulimwengu wa mapenzi.

KWA NINI WALIACHANA?
“Ali akawa staa. Alipokwenda nje nikasikia wanawake wanamshobokea. Sasa mimi sikutaka karaha nikakaa pembeni lakini jamaa ni mtu poa sana na tukikutana tunasalimiana freshi kabisa.

DIAMOND VIPI?
“Ni kweli niliwahi kuwa na Diamond (msanii wa Bongo Fleva, Nasibu Abdul). Tulikuwa na uhusiano lakini pia alikuwa mshirika wa kibiashara (hataki kuitaja). Yeye alikuwa hawezi kulala bila kuniona, lakini tulikaa kama mwezi mmoja, kwa sasa amebaki kuwa rafiki yangu na siyo mpenzi tena kama zamani,” alisema Wolper.

VIPI KUHUSU JUX?
“Jux (msanii wa Bongo Fleva, Juma Khalid) nilikuwa naye kabla ya Dallas na yule mwanaume wangu niliyeachana naye wakati wa Dallas. Katika maisha yangu nilimpenda sana Jux. Siyo marioo ni mwanaume mtafutaji aliyejiamini. Kwa sasa sipo naye. Dallas pia alichangia mimi kuachana na Jux,” alimalizia Wolper ambaye kwa sasa ana mwanaume asiyependa kumwanika.

Baada ya kulinasa Penzi la BOND, Wastara aonywa kuhusu Ngono za Kinyume na Maumbile (KABANG)...!!

Msanii nyota kwenye kiwanda cha Bongo muvi Wastara amepewa tahadhari kubwa na mshabiki wake kuhusu mpenzi wake mpya ambae ni prodyuza wa filamu aliyefahamika kwa jina la Bond Bin Sinnon kuwa amekuwa akipenda sana mapenzi kinyume na maumbile hakuna mfano.

Habari za uhakika zilitua ndani ya ofisi  zilizopo Mwananyamala Komakoma zilisema Bond ambae aliwahi kuwa na mahusiano ya kimapenzi kwa zaidi ya Miaka 4 na nusu na Mtangazaji Lulu Semagongo ambae kipindi flani aliwahi kukiri kwenye vyombo vya habari hasa magazeti pendwa kuwa yeye mzuka wake ni kufanya mapenzi na maumbile tangu akiwa mdogo.Hivyo basi hali imetiliwa shaka na mashabiki wa Wastara kuwa kwa vile wawili hao wameonekana kuwa na mahusiano ya kimapenzi basi ni dhahiri kuwa Wastara wame makini la sivyo kijana huyo anaweza kuendeleza tabia yake hiyo aliyokuwa anaifanya kwa Lulu.  

Chanzo chetu kiliendelea kuilza Xdeejayz kuwa Bond ambae tangu aachane na Lulu hakuwahi kuwa na mpenzi hata siku moja" Huyo Bond anaogopwa sana na mabint kwa sababu ya kauri ya Ant Lulu alipotangaza kuwa yeye mzuka wake ni  kifanya mapenzi kinyume na maumbile hivyo hakuna msichana yeyote anaemkubari kwa hofi hiyo hivyo hata Wastara tunashangaa wamepatana kiasi hicho"

Kilisema chanzo hicho.Mahusiano ya Bond na Wastara yalianza kwa siri sana lakini hivi sasa kila kitu wazi hadi ndugu wa Wastara wanamjua bond kama shemeji yao, 


Msanii nyota kwenye kiwanda cha Bongo muvi Wastara amepewa tahadhari kubwa na mshabiki wake kuhusu mpenzi wake mpya ambae ni prodyuza wa filamu aliyefahamika kwa jina la Bond Bin Sinnon kuwa amekuwa akipenda sana mapenzi kinyume na maumbile hakuna mfano.

Habari za uhakika zilitua ndani ya ofisi  zilizopo Mwananyamala Komakoma zilisema Bond ambae aliwahi kuwa na mahusiano ya kimapenzi kwa zaidi ya Miaka 4 na nusu na Mtangazaji Lulu Semagongo ambae kipindi flani aliwahi kukiri kwenye vyombo vya habari hasa magazeti pendwa kuwa yeye mzuka wake ni kufanya mapenzi na maumbile tangu akiwa mdogo.Hivyo basi hali imetiliwa shaka na mashabiki wa Wastara kuwa kwa vile wawili hao wameonekana kuwa na mahusiano ya kimapenzi basi ni dhahiri kuwa Wastara wame makini la sivyo kijana huyo anaweza kuendeleza tabia yake hiyo aliyokuwa anaifanya kwa Lulu.
 

Chanzo chetu kiliendelea kuilza Xdeejayz kuwa Bond ambae tangu aachane na Lulu hakuwahi kuwa na mpenzi hata siku moja" Huyo Bond anaogopwa sana na mabint kwa sababu ya kauri ya Ant Lulu alipotangaza kuwa yeye mzuka wake ni  kifanya mapenzi kinyume na maumbile hivyo hakuna msichana yeyote anaemkubari kwa hofi hiyo hivyo hata Wastara tunashangaa wamepatana kiasi hicho" Kilisema chanzo hicho.Mahusiano ya Bond na Wastara yalianza kwa siri sana lakini hivi sasa kila kitu wazi hadi ndugu wa Wastara wanamjua bond kama shemeji yao,

Michael Elizabeth 'Lulu' Katika Muonekano Mpya[Picha]

Msanii Lulu ni msanii wa Bongo movies na anajivunia kwa kuwa juu ya Gem akiwa na umri mdogo. Cheki picha alizoziweka Instagram akiwa amevalia nguo nyeupe na hairstyle mpya kabisa.





RAYUU AMWAGA RADHI HADHARANI NA MPENZI WAKE,WACHEKI HAPA[PICHA]



WAKILA BATA KWA RAHA ZAO



HUYU NDO JAMAA MWENYEWE ANAYE KAMATIA MZIGO

MWANAMUZIKI DIAMOND PLATNUMZ BAADA YA KUTANGAZA AJIRA SASA AMTANGAZA DEMU ANAYEMPENDA,Mcheki Hapa


UKIFIKA katika mtaa anaoishi mwanamuziki Diamond maeneo ya Sinza Mori jijini Dar es Salaam utaanza kuhisi kuwa kuna staa anayeishi maeneo hayo, macho ya wengi huanza kumtazama mtu anayeelekea katika geti la nyumba anayoishi msanii huyo. (HM)

Muda wote geti hilo limefungwa. Ili uweze kuingia ndani itakulazimu ubonyeze kengele itakayoashiria kuwa kuna mgeni nje anahitaji kuingia ndani. Hata hivyo hauwezi kupenya kirahisi ndani hadi uulizwe shida yako na kama hauna miadi na mtu yeyote anayeishi ndani ya nyumba hiyo haitakuwa rahisi kuingia.

Mwanaspoti lilitinga katika nyumba ya msanii huyo

na kushuhudia ukimya wa hali ya juu ilhali kuna watu ndani. Baada ya kufunguliwa geti tuliingia ndani na kupokewa na Diamond aliyekuwa ameketi katika sebule iliyonakshiwa na mapambo makini ukutani huku ikiwa na samani chache lakini za gharama kubwa.

Tulitumia saa mbili mfululizo katika mahojiano na Diamond ambaye alifunguka kwa kila swali aliloulizwa na kujibu kwa ufasaha na ufafanuzi mpana.

Mwanaspoti: Utendaji kazi wako ukoje katika muziki?

Diamond: Nina mipango makini katika kazi zangu. Mambo yote lazima yapitie kwa meneja wangu ndipo yanifikie mimi, mara nyingi mtu hawezi kuzungumza na mimi moja kwa moja lazima apite huko na hiyo ndiyo staili ya Diamond. Nimejipanga kuhakikisha nafanya kazi gani, kwa wakati gani na sikurupuki tu, japo katika utengenezaji wa nyimbo zangu naweza nikapata wazo basi hapo hapo nikatengeneza mistari.

Mwanaspoti: Utendaji kazi wako ukoje kuanzia asubuhi hadi jioni?

Diamond: Saa tano asubuhi, nikishaamka kitu cha kwanza ni kwenda 'gym', mara nyingi ni hapa nyumbani kama unavyoona hapo nje kuna sehemu ya mazoezi na sehemu

nyingine zilizopo ndani, mara nyingi hutumia muda wa saa moja. Ifikapo saa sita na nusu huwa naanza kufanya kazi zangu lakini itategemea na ratiba zangu za siku ambazo ndio mwongozo wangu wa kuimaliza siku. Baada ya hapo napumzika kwa muda fulani na baadaye jioni huendelea na kazi na mara nyingi kazi zangu huwa nazimaliza usiku wa manane.

Mwanaspoti: Unalala saa ngapi? Na unalala kwa muda gani?

Diamond: Muda wangu wa kulala mara nyingi ni saa kumi na moja alfajiri na kama sikuwa na kazi nyingi studio basi nitalala saa nane usiku. Muda wangu wa kulala ni saa sita mpaka nane kwa siku. Ila hata kama nikilala mapema kuamka ni saa tano asubuhi ila itategemea na nini ninakifanya siku inayofuata na kama nina kazi maalumu na ya mapema itanilazimu niamke mapema ili kuzikamilisha.

Mwanaspoti: Shughuli gani zinazokuchelewesha mara kwa mara kulala?

Diamond: Ni kurekodi na wakati mwingine shoo. Kwa wiki ninafanya shoo nyingi, kama ni tatu basi siku zote tatu nitalala alfajiri. Siku nyingine zinazosalia ninalala usiku wa manane kwa kuwa huwa nakuwa studio na sehemu nyingine ambazo hunilazimu kufanya kazi kwa kipindi kirefu usiku.

Mwanaspoti: Kati ya usiku na mchana ni muda upi unaopenda kurekodi?

Diamond: Kazi zangu narekodi usiku na ndiyo muda ninaopendelea zaidi. Mara nyingi napenda kurekodi saa 7 usiku ili niwe na muda na saa nyingine ni kuepuka lawama kurekodi mchana, kwasababu vijana wengi chipukizi wataona napendelewa. Unajua ninapoingia studio napenda kufanya kazi kwa muda mrefu, hata hivyo iliyo bora sifanyi bora liende na siwezi kufanya kazi na prodyuza anayenipeleka tu, ni lazima na mimi nipime kama kazi niliyoifanya inakwenda vile ninavyotaka au kama yeye anavyotaka ilimradi tufanye kazi nzuri na iliyo

bora.

Mwanaspoti: Unatumia muda gani kurekodi singo moja na kwa upande wa video ni siku ngapi?

Diamond: Inategemea, inaweza kuwa siku mbili au miezi sita lakini nyimbo nyingi zinatumia muda mwingi kwasababu wakati mwingine naanza halafu napata shoo hivyo inanibidi nipange muda mwingine wa kurekodi. Kuna nyimbo zangu ambazo nilizifanya kwa muda mrefu sana hizo huwa sizisahau ikiwemo Ukimwona, Mbagala, Nataka Kulewa na nyinginezo. Nakumbuka katika kazi nilizofanya kwa muda mfupi ni My Number One nilioufanya kwa prodyuza Sheddy Clever kwa kipindi kifupi sana pamoja na Mapenzi Basi sambamba na Binadamu hizi ni baadhi ya kazi ambazo hazikunipasua sana kichwa kuzikamilisha.

Mwanaspoti: Una prodyuza wako maalumu au studio yako mwenyewe?

Diamond: Sina prodyuza maalumu kila kazi nitakayotaka kuifanya ninatafuta prodyuza yule ninayemtaka hata kama sijawahi kufanya naye kazi. Ninafanya hivi nikiwa na malengo maalumu kwa kujiweka vizuri mimi kama msanii na hata kuwapa nafasi maprodyuza mbalimbali kutia mkono kwenye kazi ya mikono yangu. Ninaogopa kuwa na prodyuza maalumu kwa kuwa najua atanisumbua ikiwa atajua kwamba namtegemea yeye pekee katika kazi zangu. Studio sina kwa sasa ila nina mikakati ya kuwa na studio kwani nimeshanunua baadhi ya vifaa.

Mwanaspoti: Unadhani ndiyo sababu iliyokufanya ukagombana na Bob Junior au Manecky?

Diamond: Hapana haya mambo yalishapita lakini nilijifunza mengi ndiyo maana niliamua kuja na staili hii. Naogopa kubaki kuwa msanii ninayetegemea prodyuza fulani, bila yeye siwezi kufanya muziki, lakini mimi ni Diamond ninaweza kufanya muziki na prodyuza yeyote naye akaonyesha ufundi wake kupitia kazi yangu.

Mwanaspoti: Shoo gani kubwa kuliko zote uliyowahi kufanya ambayo haijawahi kujirudia?

Diamond: Diamond Forever. Hii ilikuwa kubwa sana ambayo sitakaa nikaisahau, ilihudhuriwa na watu wakubwa na maarufu hapa nchini hata hivyo ilikuwa ya kipekee ambayo haijafanana na yoyote ile. Ya pili ni ile ya Dar Live ambayo nilifanya baada ya kushuka katika helikopta ile pia ilikuwa kubwa. Lakini kwa nje ya nchi ni Mombasa na Comoro huko nilifanya shoo kubwa sana ambazo siwezi kuzisahau.

Mwanaspoti: Ni shoo ipi iliyowahi kukuingizia pesa kubwa kuliko zote?

Diamond: Shoo ile ya Mlimani City ya Diamond Forever, ile iliniingizia pesa kubwa sana na tangu pale ndipo nilipoanza kufurahia matunda ya kazi yangu. Nilifanya shoo pia Burundi, Mombasa na Congo shoo hizi ziliniingizia kiasi kikubwa sana cha pesa siwezi kutaja ni shilingi ngapi lakini ni pesa nyingi ambazo sitakaa nizisahau.

Mwanaspoti: Shoo ipi ilikuwa ya bei chee ambayo huwezi kuisahau

Diamond: Kwa kweli siwezi kusahau nilipofanya shoo yangu ya kwanza kubwa mwaka 2009 kwenye Fiesta iliyofanyika Dar es Salaam, ilikuwa ndiyo shoo yangu ya kwanza na kubwa wakati huo nilikuwa natamba na wimbo Kamwambie, ilinichukua muda mrefu sana kujiandaa mimi pamoja na madansa wangu wanne tulilipwa Sh 50,000 lakini sikukata tamaa kwani ilikuwa ndiyo mwanzo wangu wa kujuana na watu wengi na wadau wakubwa wa muziki hapa nchini ambao nilikutana nao kwenye ile shoo.

Mwanaspoti: Kwa hivi sasa ni shoo gani ambayo unaweza kusema kwamba utafanya kwa bei ya chini na ni shilingi ngapi?

Diamond: Shoo ninayoweza kufanya kwa bei ya chini kabisa ni Sh 10 milioni za Kitanzania na hii labda nione anayeniomba nifanye shoo hiyo hayuko vizuri na pengine ni rafiki yangu na hawezi kuninyonya, si hivyo tu itategemea pia ni kampuni gani na ni watu wa aina gani ambao watanitaka nifanye nao kazi.

Mwanaspoti: Kwa kawaida Diamond ni msanii wa gharama gani kwa shoo moja ndani na nje ya nchi?

Diamond: Kwa kawaida shoo moja ninafanya kuanzia Sh15 milioni mpaka Sh20 milioni kulingana na muda nitakaofanya shoo. Pia zile za nje ninafanya kwa gharama ya Dola 20,000 mpaka 30,000 yaani ni Sh32 milioni mpaka 48 milioni hivi kwa fedha za Tanzania na nikiwa huko nahakikisha ninafanya kazi vile inavyotakiwa. Lakini hali ni tofauti inavyokuja shoo ile ya uwanjani yaani hapa nazungumzia shoo kubwa zinazofanyika nje ya ukumbi, hizi natoza Dola 20,000 ambayo ni sawa na Sh32 milioni 32 kwa fedha ya Kitanzania.


Mwanaspoti: Kuhusu madansa wako unawachukuliaje?

Diamond: Ni kama kaka zangu na ninawapenda sana kwani tumetoka nao mbali na wanajua kuwa tunafanya kazi pamoja kutengeneza maisha hivyo ni kama ndugu zangu na tunasaidiana kwenye kila jambo ukizingatia kuwa kile tunachokipata tunagawana. Kwa kweli najitahidi sana kuwaambia hasa kuhusiana na masuala ya kimaisha, nahusika katika maisha yao ya kila siku na nijuavyo mimi nikikosea tu mmoja akapotea kundi langu litakuwa limeharibikiwa maana kila mtu namtegemea kwa upande wake. Kwa sasa wamejenga nyumba zao na wanaendelea vizuri kimaisha hilo ndilo sharti langu lazima wafanye mambo ya maendeleo kwa kile tunachokipata.

Mwanaspoti: Umesafiri nao nchi ngapi, na kwanini unapenda kuambatana nao?

Diamond: Nimesafiri nao sehemu mbalimbali kama Burundi, Comorro na sehemu nyinginezo ambako nimekwenda kufanya shoo, sina tabia ya kusafiri peke yangu hata nikienda Ulaya na hata Marekani lazima niwe nao. Ninapenda kuwa nao kwani ni sehemu ya muziki wangu na imefika wakati nimekuwa nataka mapromota kuhakikisha wanatulipia mimi na madansa wangu kwa ajili ya shoo hasa tutakapojua kuwa shoo fulani itaingiza watu wengi au udhamini mkubwa.

Mwanaspoti: Kuna safari ambayo umewahi kusafiri peke yako?

Diamond: Ziko nyingi, nilienda mwenyewe kutokana na ukubwa wa shoo, lakini ni miaka kadhaa nyuma, baadaye nilijiwekea mikakati kwamba siwezi kusafiri mwenyewe wakati shoo nahitaji kufanya na madansa wangu, awali mapromota walikuwa wagumu kunielewa na wapo waliokataa. Niliachana nao na kuwataka wakishajipanga na kuhakikisha kwamba wanaweza kunichukua mimi na madansa wangu watafanya hivyo.

Mwanaspoti: Umewahi kuwatema madansa?

Diamond: Sijawahi kubadilisha madansa kwa sababu wanajua kazi yao. Ingawa nilikuwa na madansa sita nilipokuwa naanza muziki lakini niliachana na wawili kutokana na utendaji wao wa kazi. Wawili hawa hawakuwa wabunifu kila siku walikuwa na staili ileile, niliamua kuchagua vichwa ambavyo vikikaa na mimi mwishowe tunatoka na kitu makini na chenye kueleweka. Kulikuwa na tatizo pia la kukosea stepu wakati wa shoo hili lilikuwa likinishushia sana hadhi yangu jukwaani, hapo ndipo nilipoamua kuwaondoa.

Mwanaspoti: Kwa upande wa malipo unawalipaje?

Diamond: Ninawalipa vizuri lakini siwezi kutaja kiwango ila ingekuwa kwangu ningetaja, hiyo ni haki yao wao wenyewe kutamka ila mimi siwezi kutaja. Malipo ninayowalipa yapo machoni mwa watu wanaowazunguka, dansa kujenga nyumba kumiliki baadhi ya biashara si jambo dogo, hivyo ninawalipa vizuri. Na hata gharama za kusafiri ndani na nje ya nchi vyote ni juu yangu, malipo tunayoyapata tunagawana.

Mwanaspoti: Unakumbana na changamoto zipi katika kazi yako?

Diamond: Nakumbana na mengi, kwanza unapokuwa msanii unayeongoza lazima upate vikwazo vingi. Nakumbana na watu wengi wanaonichukia na kunitusi bila sababu za msingi, hata hivyo nasingiziwa vitu vingi ambavyo havipo nadhani hii ni changamoto iliyotokana na kufanya vizuri katika muziki.

Wapo ambao wanamwona Diamond anafanya vizuri kwenye muziki badala ya kukaa na kuangalia nimepita wapi na wapi anaanza kutoa lawama kwamba ameibiwa na mengine ambayo kimsingi hayana maana.

Mwanaspoti: Siku za hivi karibuni kuna maprodyuza na wasanii wasiofahamika ambao walijaribu kutengeneza kazi yako ya My Number One na kukutusi kupitia wimbo huo na wapo waliotunga mashairi mengine yaliyozungumzia maisha yako kabla hujawa staa, ulijisikiaje? Na unachukua hatua gani?

Diamond: Awali niliumia sana nilipoibiwa mashairi ya wimbo wangu wa Mbagala, iliniuma sana kwa muda wa wiki nzima uchungu nilioupata siwezi kuuelezea. Lakini baadaye nilikomaa, huwezi amini niliposikia zile nyimbo nilicheka sana kisha nikawadharau sana watu waliofanya hivyo maana nipo kwenye hii tasnia siwezi kuchukia watu wasiojua walitendalo kwani na wao wapo katika kujitafutia riziki. Lakini hata hivyo sheria ya muziki bado haijawa makini hapa nchini

nitachukua hatua gani mwisho wa siku nitaacha kufanya mambo yangu ya msingi na kushughulikia wezi wa kazi zangu ambao hata hivyo hawatabanwa kwa lile walilolifanya.

Mwanaspoti: Msanii yupi hapa Tanzania anakutisha kama hayupo vipi huko nje ya nchi?

Diamond: Kwa hapa Tanzania sijaona mwanamuziki anayenitisha, ila siwezi kujua mashabiki wao ndio majaji, nafikiri kila mtu anaweza kuwa na mtazamo wake. Kati ya wanamuziki ninaowahusudu mimi kwa nje ya nchi hasa Afrika ni P Square pekee, hawa wapo katika nafasi kubwa sana kwenye ubongo wangu na nafikiria ni lini ninaweza kuwafikia, hiyo ndiyo ndoto yangu daima.

Mwanaspoti: Unapokuwa juu ya jukwaa unakumbana na vishawishi vipi ukiwa kama msanii mkubwa?

Diamond: Ninapata vishawishi vingi sana ninapokuwa jukwaani. Kwa kweli ninashawishiwa na wakinadada, mfano kuna mwanamke mmoja ambaye alikuwa mmoja wa mapromota wa shoo nchini Uingereza alitaka kunibusu mdomoni kwa lazima, kitendo kile kilinifedhehesha sana na nilishindwa nifanyeje kwani nipo ugenini na jukwaani ilikuwa ngumu sana kwangu. Wakati mwingine wanawake wanapanda jukwaani ili wacheze na wewe mwisho wa siku wanaingiza mikono kwenye suruali yaani sipendezwi kabisa na michezo ya namna hii.

Mwanaspoti: Umewahi kuibiwa ukiwa jukwaani?

Diamond: Nimeshaibiwa sana hasa katika hizi shoo ndogo ndogo mara nyingi watu wanapanda jukwaani na kuondoka na kitu chako. Nakumbuka nimeshawahi kuibiwa saa, pete ya dhahabu na kuna mmoja alitoa kali ya mwaka yaani yeye alinivua nguo kwa lazima.

Mwanaspoti: Inakuwaje nje ya muziki, unakumbana na changamoto zipi?

Diamond: Kitu ambacho ni changamoto kubwa sana kwangu ni simu yangu ya mkononi. Kila baada ya miezi sita au mitatu nalazimika kubadili namba yangu ya simu, nasumbuliwa sana na watu ambao hata hivyo hawana la msingi la kuniambia. Ni kweli kwamba mawasiliano ni kitu cha msingi na 

ninawapenda mashabiki wangu lakini namba yangu inasambaa kwa kasi ya ajabu kiasi kwamba nashindwa kupokea simu za maana kwa kudhani kwamba na hao nao ni wasumbufu.

Mwanaspoti: Ina maana milio yote ya simu hapo ni watu wanakupigia?

Diamond: Yap, unavyoona inalia kila dakika watu wanapiga hapa. Muda mwingi hii simu ninaweka 'silent' yaani haitoi mlio wowote kwani inaita kila dakika.

Mwanaspoti: Tuzungumzie uhusiano wako. Mpenzi wako wa kwanza unamkumbuka? na je uliwahi kumpa shilingi ngapi?

Diamond: Mpenzi wangu wa kwanza kabisa enzi hizo ninajifunza mambo haya sikumbuki vyema jina ila alikuwa anaishi Tandale na mimi pia nilikuwa naishi huko na mama yangu. Sikumbuki kama nimewahi kumhonga maana enzi hizo mimi nilikuwa napewa tu na mama yangu pesa, sikuwa na hela yoyote ya kumpa na ilikuwa ni kwa kipindi kifupi kama miezi minne hivi, hata hivyo tulikuwa tunaibana tu kwa siri nilikuwa mdogo.

Mwanaspoti: Kwanini mliachana?

Diamond: Kwanza nilikuwa sijajua mapenzi ni nini. Hata hivyo haikuwa rasmi na wala nilikuwa sijawa na akili ya kupenda sana na nilikuwa na fikra kwamba ni mchezo tu hivyo tuliachana mapema kwani hata yeye akili yake ilikuwa haijakomaa.

Mwanaspoti: Mpenzi wako uliyekuwa naye kabla ya kuwa staa nasikia uliachana naye baada ya kutoka kimuziki kwa nini?

Diamond: Nilimpenda sana lakini aliniacha kabla ya kutoka. Mpenzi wangu wa kwanza alikuwa anaitwa Sarah Sadick, sijawahi kumuhonga na ndiye mwanamke niliyewahi kumpenda sana. Wakati huo Naseeb Abdul kabla sijawa Diamond nilikuwa nahaha kuhangaika ni vipi nitatoka kimuziki. Msichana huyu ndiye aliyenipa hasira za kufanya muziki kwa bidii zote baada ya kunitema na kuanza kuhangaika na wengine na aliniita majina mengi yasiyo mazuri, kisa sina fedha. Si kwamba nilimuacha bali yeye ndiye aliyeniacha kama zali baada ya wiki kadhaa nikatoka na wimbo Kamwambie, taratibu nikaanza kuwa staa naye akaanza kurudi ila nilishamuondoa moyoni mwangu.


Mwanaspoti: Kwa nini mliachana? Unadhani hakukufaa tena kwa kuwa ulishakuwa staa?

Diamond: Alinisumbua sana kutokana na ugumu wa maisha niliokua nao kwa kipindi cha nyuma hadi kufikia 2009. Nilimpenda sana huwezi amini nilikuwa silali usingizi kwa ajili yake. Nahisi ilitokana na mimi kukosa kazi ndiyo maana ilifikia hatua alinipotezea. Lakini baada ya kupata na kujulikana alinifuata lakini sikutaka tena hata baada ya kuniomba msamaha.

Mwanaspoti: Umewahi kuwa na wanawake wangapi tangu uwe staa?

Diamond: Sikumbuki kwa kweli wapo wengi mno, si unajua tena wapo walionitaka na kunilazimisha nifanye hivyo, lakini idadi kamili siwezi kukumbuka na kila siku nasumbuliwa na hawa wanawake.

Mwanaspoti: Ni wapenzi wangapi ambao umekuwa nao kipindi kirefu na kuwapenda kama wapenzi wako?

Diamond: Nimewahi kuwa na wapenzi wanne katika kipindi chote cha ustaa wangu na sikupenda kubadili ovyo ila wengi wao hawakuweza kutimiza haja ya moyo wangu.

Mwanaspoti: Unaweza kuwataja majina?

Diamond: Ndiyo ila wawili wanafahamika zaidi. Wa kwanza kabisa alikuwa anaitwa Sarah na wa pili alikuwa anaitwa Hawa yule msichana niliyeimba naye katika wimbo 'Nitarejea', huyu alizidiwa ujanja na Wema Sepetu ambaye naye alikuja kuondoka kwangu na baadaye nikawa na Penieli Mungilwa.

Mwanaspoti: Mwanamke yupi unahisi ulimpenda kuliko wote?

Diamond: Mwanamke wangu wa kwanza Sarah Sadick huyu aliniingia sana moyoni sijajua ni kwanini. Lakini nahisi huenda kwa kuwa awali alinipenda kweli kwa kuwa wakati huo sikuwa na kitu. Hata hivyo nahisi ilitokana na mimi kutokuwa bize na wakati huo sikufikiria lolote zaidi ya yeye ilitokana na kutokuwa na kazi ya kufanya. Siku hizi sina mapenzi ya kivilee, nawaza zaidi pesa na ninaihangaikia na zaidi ni muziki wangu, hili ndilo la kwanza kabisa linalonifanya niwe bize mapenzi baadaye.

Mwanaspoti: Umeshawahi kutongozwa na wanawake?

Diamond: Ndiyo, wengi sana tena kuna mmoja kati ya wanawake niliowahi kuwa nao alinitongoza yeye mwenyewe ndipo nikawa naye na nilikaa naye katika uhusiano kwa kipindi kirefu tu. Wanaweza kumfikiria mwanamke fulani lakini huwezi amini ukweli ninao mimi mwenyewe na katu hawawezi hata kumhisi. Ninatongozwa sana kwenye mitandao ya kijamii, facebook, whatsapp, Instagram na kwingineko na wapo wasichana ambao wanatafuta namba zangu za simu na kuanza kunisumbua.

Mwanaspoti: Unapata usumbufu wowote toka kwa wanawake?

Diamond: Ndiyo, wengi sana tena kuna mmoja kati ya wanawake niliowahi kuwa nao alinitongoza yeye mwenyewe ndipo nikawa naye na nilikaa naye katika uhusiano kwa kipindi kirefu tu. Wanaweza kumfikiria mwanamke fulani lakini huwezi amini ukweli ninao mimi mwenyewe na katu hawawezi hata kumhisi. Ninatongozwa sana kwenye mitandao ya kijamii, facebook, whatsapp, Instagram na kwingineko na wapo wasichana ambao wanatafuta namba zangu za simu na kuanza kunisumbua.

Mwanaspoti: Ni mwanamke wa aina gani unataka awe mkeo?

Diamond: Kwanza ninahitaji aijue kazi yangu na ajue kwamba mimi ni mtu maarufu hivyo akubaliane na changamoto mbalimbali atakazokumbana nazo kwa kipindi atakachokuwa ndani ya ndoa, siyo siku mbili anafungasha virago. Pia ajue kwamba nitamsikiliza mama yangu kwanza kabla ya yeye hilo naliweka wazi, yeye ana nafasi yake katika maisha yangu lakini mama yangu nimempa kipaumbele, tatu awe tayari kuishi na mama yangu. Nne awe na akili na mwenye utambuzi na atakayeniongoza katika kazi zangu, sihitaji. Itaendelea… 
Chanzo: mwanaspoti