Kila
anapopanda jukwaani huambatana na ‘pacha’ wake wanaopamba maonyesho
yako, kuongeza ladha ya muzikin wake. Huyu siyo mwingine bali ni msanii
wa muziki wa mduara, Snura Mushi
anayetamba
na wimbo Nimevurugwa, baada ya wimbo wa Majanga aliourekodi mwishoni
mwa jana. Snura anamiliki madansa wanne ambao ni Farida na Faidha
Jafari, hawa wasichana. Lakini pia anao wacheza shoo wa kiume; Elisha na
Eliya Askofu.
Siyo
rahisi kuwatofautisha madansa hao mahiri kutokana na kufanana,pia
kuonyesha kuipenda kazi yao na kuithamini wakiwa na viwango sawa vya
uchezaji.
Baadhi
ya mashabiki waliowahi kuhudhuria maonyesho Snura, bila shaka hupata
wakati mgumu kuwatofautisha madansa hao kwa kuwa mfanano wao ni kuanzia
miili, uchezaji hadi nguvu wanazozitumia kwa pamoja wawapo jukwaani.
Starehe
lilimtafuta Snura ili kujua kwa undani kuhusu uamuzi wake wa kufanya
kazi na pacha hao na alipowapata, ambapo alianza kwa kueleza kuwa
binafsi alitumia zaidi ya mwezi mmoja kuweza kuwatofautisha.
Mwandishi: Madansa wako mbona wanafanana sana kiasi cha kushindwa kuwatofautisha?
Snura:
Nina madansa wanne. Hawa ni pacha wa mfuko mmoja,wasichana walizaliwa
katika familia ya Mzee Jafari, wavulana wanatoka katika familia ya
Askofu.
Mwandishi: Kwa nini uliamua kuchukua pacha na kuwaajiri kama madansa wako?
Snura:
Ilitokea tu. Awali, nilikuwa na madansa lakini waliondoka na nikabaki
na mmoja. Nikaamua kutafuta mwingine mmoja wa kike na bahati nzuri
nilipata wawili ambao ni pacha. Niliamua kuwachukua wote, hata hivyo
yule mmoja hakudumu akaondoka nikabaki na hawa wawili ambao ni pacha.
Siku isiyo na jina meneja wangu alinipigia simu na kuniambia kuwa
amepata pacha wengine hivyo niongeze idadi ya dansa. Nilikubali na mara
nilipokutana nao nilistaajabu kuona nao wamefanana sana.
Mwandishi: Unawezaje kuwatofautisha?
Snura:
Mwanzoni ilikuwa ngumu ilinichukua muda mrefu kuwajua na kutofautisha.
Ilifikia hatua nikimwita Farida nahisi amekuja Faidha,vivyo hivyo kwa
hawa wavulana, lakini sasa kuna alama ambazo zinanitambulisha, naweza
kuwatofautisha. Ila wenyewe wanapenda kusuka sare hata wale wa kiume nao
wananyoa kiduku wote wawili ni ngumu kwa aliye mbali nao
kuwatofautisha.
Mwandishi: Imewahi kutokea pacha hawa wakagombana, huwa unachukua hatua gani katika kuwasuluhisha?
Snura:
Mapacha wanajulikana tabia zao. Kugombana wanagombana, tena inaweza
kutokea wakaanzisha ugomvi muda mbaya, unaona tunakwenda kufanya shoo
wanaanza kugombana hadi tunaingia kwenye gari, ila mimi huwawafokea kwa
kuwa sipendi wagombane.
No comments:
Post a Comment