Social Icons

Dondosa Twitter Facebook

Thursday, January 9, 2014

KITUO CHA BBC NCHINI UINGEREZA CHA MTAJA DIAMOND PLATNUMZ NI MSANII ATAKAE FANYA VIZURI SANA BARANI AFRICA MWAKA HUU (2014)

http://laivu.com/maraha/files/2013/04/diamond-platnumz-l.jpg
DJ wa kituo cha radio maarufu kwa burudani nchini Uingereza kilicho chini ya shirika la habari la Uingereza, BBC cha BBC Radio 1Xtra, DJ Edu, amemtaja Diamond Platnumz, miongoni mwa wasanii watano wenye dalili za kufanya vizuri barani Afrika mwaka 2014.

Sio Diamond Plutnumz Pekee aliyetawa bali wasanii wengine waliotabiriwa kufanya vizuri Afrika ni pamoja na Kaysha,(msanii wa DRC aishie Ufaransa), Wyre wa Kenya, Radio na Weasel wa Uganda na King James wa Rwanda.

JACK PATRICK ALIYEKAMATWA NA MADAWA YA KULEVYA MAPYA YAIBUKA


Jacqueline Patrick ‘Jack’.

Mrembo huyo alikamatwa Desemba 19, mwaka jana katika Uwanja wa Ndege wa Macau akitokea Bangkok, Thailand akiwa na kete 57 (kilo 1.1) za unga aina ya heroin tumboni zikiwa na thamani ya shilingi milioni 300. 
TAARIFA MBICHI
Taarifa mbichi kabisa zinadai kwamba, Jack amepewa mwaka mmoja na nusu (siku 447) ajifunze lugha inayozungumzwa na watu wa Macau (Kireno) ambayo ndiyo itakayotumika mahakamani wakati kesi yake itakapoanza kuunguruma.

 
Dawa za kulevya alizokutwa nazo Jack Patrick.

Sheria ya kisiwa hicho inasema kuwa mshitakiwa yeyote atakayefikishwa kortini, kesi yake haitasikilizwa mpaka majaji wakubali kwamba anajua lugha hiyo na si kinyume na hapo.
Kwa mujibu wa vyanzo hivyo, mwalimu maalum anayejua Lugha za Kiingereza na Kireno ndiye atakayemfundisha Jack mpaka atakapojua.
AKIJUA MAPEMA ITAMSAIDIA
Habari za ndani kutoka vyanzo vya uhakika nchini humo zinasema kwamba, kama Jack angekuwa anakijua Kireno angepandishwa kizimbani mara baada ya upelelezi kukamilika, Machi mwaka huu.
KIFUNGO CHA CHINI MIAKA 16
Habari nyingine mpya kutoka Macau zinasema kuwa, sheria za eneo hilo kuhusu makosa ya kukutwa na madawa ya kulevya, mtuhumiwa akitiwa hatiani kifungo cha chini ni miaka 16 kulingana na mwenendo wa kesi.
SERIKALI YA TANZANIA YASUBIRI ORODHA…
Juzi, Uwazi liliwasiliana kwa simu ya mkononi na Kamanda wa Kikosi cha Kuzuia na Kupambana na Madawa ya Kulevya Tanzania, Godfrey Nzowa na kumuuliza kuhusu nini kinaendelea kati ya serikali na utawala wa Macau kufuatia Mtanzania, Jack Patrick kunaswa na unga nchini humo.
Nzowa: “Aaah! Sisi tumetuma maswali yetu kule (Macau) kupitia Polisi wa Kimataifa (Interpol), tumetaka kujua kama huyo binti (Jack) amewataja vigogo waliomtuma ni majina gani wanayo.
“Ndiyo tunasubiri majibu yao ili tujue nini kinaendelea kule. Kama aliwataja watu tutaanza kuwafuatilia mara moja maana lazima kuna vigogo nyuma yake.”
KWA NINI MABOSI WA KUBEBA UNGA HUWA HAWATAJWI?
Kinachomshangaza Kamanda Nzowa ni usiri wa watu wanaodaiwa kukamatwa na unga kufunga vinywa vyao kuwataja vigogo waliowatuma.
Inadaiwa moja ya kiapo kikubwa kabla mtu hajaanza kuwa ‘punda’ (kubebeshwa madawa ya kulevya) ni kusema ‘piga, ua, galagaza’ katu hawezi kutaja wahusika wenye mzigo.
“Unajua kwa sababu gani? Wale wanaobeba wanaambiwa mkikamatwa msitutaje hata iweje ili tufanye mipango ya kuwatoa. Sasa mtu anaona nikitaja sintatoka, ndiyo anaamua kuendelea kuishi na siri yake halafu na wao wakubwa wao wanakuwa hawana habari nao,” alisema Nzowa.

KUMBE JACK ALIPEWA MAJI YA MOTO
Habari zaidi zinasema kuwa, siku ya tukio la kukamatwa, Jack alikataa kwamba hajabeba kete za unga tumboni, askari wa uwanjani wakampa maji ya moto ili anywe.
“Kwa mtu aliye na kete tumboni, hawezi kukubali kunywa maji ya moto kwani huyeyusha kete zilizomo ndani na kuweza kusababisha kifo chake.
“Jack alikataa kunywa maji ya moto, hilo likachangia askari kuamini ana kete tumboni, ndiyo maana walimpeleka chooni kuzitoa kitaalam,” kilisema chanzo.
RAY C AWASHANGAZA WENGI
Kufuatia sakata la Jack, hivi karibuni, staa wa muziki wa kizazi kipya Tanzania, Rehema Chalamila ‘Ray C’ aliingiza kwenye mtandao wake wa kijamii akitoa maoni kwamba Jack apewe adhabu kali zaidi ya kifungo (pengine kunyongwa) hali iliyowashangaza wengi waliotembelea mtandao huo.
Baadhi ya watu waliozungumza na Uwazi baada ya staa huyo kuingiza mawazo yake walimshutumu wakisema alitakiwa kutafakari upya.
“Yule dada (Ray C) hakutakiwa kumtakia mwenzake mabaya zaidi, kama yeye aliathirika na madawa na amepona anatakiwa kuwa balozi kwa wengine na si kuwahukumu wenzake,” alisema Joan Mushi, mkazi wa Sinza ‘E’ jijini Dar.
WAZIRI MEMBE VIPI?
Juzi, Uwazi lilimtafuta Waziri wa Mambo ya Nchi za Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bernard Kamillius Membe ili azungumze lolote kuhusu sakata la Jack Patrick lakini hakupatikana badala  yake naibu wake, Mahadhi Maalim alisema taarifa za Jack kukamatwa amezisikia  kupitia vyombo vya habari na hana habari kiundani ila bosi wake anaweza kuwa na maelezo zaidi.
WOLPER, AUNT EZEKIEL, WEMA, WANAWINDWA KUWA ‘MAPUNDA’
Wakati Jack akiwa katika mazito hayo, habari ambazo zilifika kwenye dawati la Uwazi dakika za mwisho zinasema mastaa wa filamu za Bongo, Jacqueline Massawe Wolper, Aunt Ezekiel Grayson na Wema Isaac Sepetu wamekuwa wakitolewa udenda na vigogo wa unga. 
Vigogo hao wamekuwa wakihaha kutafuta namna ya kuwaingiza mastaa hao kwenye ‘chaneli’ yao ili wawe mapunda wa kubeba kete za unga kupeleka ughaibuni wakiamini kuwa, mastaa hawakamatwi hovyo uwanja wa ndege, hususan wa Dar es Salaam.

Rapper Wa Tanzania Naye Akamatwa Afrika Kusini Kwa Ishu Ya Madawa Ya Kulevya




Msanii chipukizi wa  HIP HOPE kutoka kibaha mkoani pwani anaye fahamika kwa jina KURUTI ARTIST atimaye amekamatwa nchini  SOUTH AFRICA ENEO LA SOWETO akiwa  ana kete 5000 za madawa ya kulevya.
Msanihi uyo aliye ondoka nchini kwa mwaliko wa watanzania waishio huko  kwa lengo  la kuenda kufanya show.
Na ndipo alipo amuakuingia kwenye bishara hiyo ili areje nayo Tanzania.akiwa uwanja wandege akijiandaa kurudi nchini ndipo maafisa usalama wa kituo chandege  wa lipo mtilia mashaka na kuamaua kumkagua na kumkuta na kete hizo zamadawa yaa kulivya na kuamua kumkamata na kumueka lumande akisubiri ukumu .

Wednesday, January 8, 2014

[Official Video] NIKKI MBISHI - PESA KWANZA


[Official Video] Diamond Platnumz Feat. Davido - Number One 'Remix'


New AUDIO | Diamond Platnumz Feat. Davido - Number One 'Remix' | Download

http://old.hulkshare.com/dl/yo2po4oxe4n4/Diamond_Platnumz_Feat._Davido_-_Number_One_%27Remix%27%5BDJMwanga.com%5D.mp3?d=1

New AUDIO | Amini - November or December | Download

http://old.hulkshare.com/dl/gn85man3n6rk/Amini_-_November_or_December_By_DJMwanga.com.mp3?d=1

Hemedy Phd Na Gelly Wa Rhymes - The One | Download

http://old.hulkshare.com/dl/el1md5c3fshs/Hemedy_Phd_Na_Gelly_Wa_Rhymes_-_The_One__By_DJMwanga.com.mp3?d=1

RAY C "BADO NIPO SINGLE JAPO BADO NASUMBULIWA SANA NA VIDUME".


 
 
Akiongea na chanzo cha habari hii, Ray C amesema picha alizoziweka Instagram akiwa na mwanaume si maisha halisi bali alitaka ‘kuhave fun’ na mashabiki wake. Lakini amekiri kuwa usumbufu anaoupata kutoka kwa wanaume si mdogo.
“Sijapata bado mchumba nilikuwa nawachombeza fans wangu kwenye Instagram kwasababu nasumbuliwa sana.”
 
Ray C yupo single.. at least kwa muda huu.
Kuhusu nyimbo mpya, Ray C amesema mwaka huu atarudi kwenye muziki kwa kuachia nyimbo mfululizo akianza na ‘Walimwengu Wote Wajue’utakaotoka mwezi March.

“Wapenzi wa muziki wangu wakae mkao wa kula,nyimbo zipo tayari bado kuziachia tu. Mwaka huu nitaanza na wimbo ‘Walimwengu Wote Wajue’ ambao umefanyikia chini ya C9 Records. Baada ya hapo harakati za muziki zitaendelea,” alisema Ray C.

Katika hatua nyingine, Ray C ameandika ujumbe huu kwenye Instagram: Yes am back……Ingawa wabaya wangu walitamani nisipone…Mungu alinipenda zaid…back to life ….am back Yo!!!Sty Tuned….Big Things are coming.

Wema Atokelezea Na Shemeji Yake Diamond..Wacha Movie Iendelee




Davido Kufanya Collabo na Msanii huyu ni Baada ya Number 1 Remix Kufanya Vizuri



Ohyeah…mapema Januari 6, Diamond Platnumz aliachia ngoma yake, “My Number One” Remix ambayo ameshirikisha Davido all the way from Nigeria . Moja ya mstari aliouimba Davido kwenye ngoma hii ni kipisi kisemacho “Tanzania to Lagos”, kinachoashiria ushirikiano mzuri kati ya nchi hizi mbili, ila safari hii, Davido ameelekeza mashambulizi ya burudani pande za ...
Uganda, kwa mkali Dr. Jose Chameleone.


Kupitia ukurasa wa Facebook wa nguli huyu wa muziki kutoka Uganda, anayetamba na kibao chake kiitwacho “Tubonge”, amewashirikisha wapenzi wa muziki na mashabiki wake furaha aliyokuwa nayo kwa kuona mwaka mpya na kudodosa kuwa kazi inayofuata atakuwa ameshirikiana na mkali huyo wa Naija, Davido.






Si hilo tu, bali Chameleone ali share kipande kidogo cha audio ya jinsi mdundo huo utakavyoskika mara baada ya kutoka.

Wema Amsifia Martin Kadinda


.
MSANII nyota wa filamu Bongo Wema Isack Sepetu amefunguka kwa kudai kuwa hawezi kuvunja urafiki na meneja wake Martin Kadinda kwa sababu kama kuna kitu chochote cha mafanikio nyuma yake yupo Kadinda.

Wema Sepetu ameuambia mtandao wa FilamCentral kuwa hana rafiki anayejua siri zake zaidi ya
meneja huyo ambaye amekuwa akimuongoza vema.

“Kadinda ndo kila kitu kwangu, hata akiondoka na kukaa mbali na mimi kwa muda mrefu ninapokutana naye tu, nitamweleza kila kitu toka siku ya mwisho tuliyoachana, hivyo inakuwa kama sijapoteana naye,yaani ni kama vile nipo naye kila siku iendayo kwa Mungu.”alisema Wema.

Msanii huyu ameendelea kusema kwamba hata kampuni yake ya Endless Fame film aliifungua kwa msaada wa Kadinda baada ya kumshauri kuwa kwa hadhi yake anastahili kuwa na kampuni na aache kuigiza filamu za watu wengine.

LULU: KAMA SI KANUMBA YANGENIKUTA MAZITO



Elizabeth Michael Kimemeta ‘Lulu’.

SURA ya mauzo katika sinema za Kibongo, Elizabeth Michael Kimemeta ‘Lulu’ ametoa ya moyoni kuwa kama siyo kuwekwa nyuma ya nondo za Mahabusu ya Segerea, Dar basi yangemkuta mazito.

Marehemu Steven Kanumba ‘The Great’.
Lulu alikaa Gereza la Segerea kwa takribani miezi kumi baada ya kutokea kifo cha aliyekuwa mwandani wake, marehemu Steven Kanumba ‘The Great’ aliyefariki dunia Aprili 7, 2012.
Nyota huyo wa Filamu ya Foolish Age alifunguka mambo ya kushangaza hivi karibuni juu ya tukio hilo kupitia Kipindi cha Take-One, kinachorushwa na Clouds TV.
TATIZO FOOLISH AGE
Lulu alikuwa akizungumzia filamu yake hiyo ya Foolish Age ambapo alisema sinema hiyo inawasihi wasichana ambao wanapitia kipindi cha balehe ambacho ni hatari sana kwao.
“Kwa kweli kipindi cha foolish age ni cha hatari sana, nilicheza filamu hiyo ili kuwaasa wasichana wenzangu.
“Asikwambie mtu, mimi mwenyewe nilikokuwa nikielekea si kuzuri kabisa.
KAMA SIYO KANUMBA
“Ukweli ni kwamba kama siyo matatizo (kifo cha Kanumba) nikaenda mahabusu sijui ingekuwaje sasa hivi. Kukaa jela kulinisaidia kusitisha kasi ya tabia yangu, nikatoka nikiwa mpya.
“Yangenikuta mazito zaidi maana kipindi kile ilikuwa hatari tupu,” alisema Lulu ambaye ni mrembo wa haja.
Staa huyo aliongeza kuwa kipindi hicho kilikuwa cha hatari na hakitamani kijirudie hata kidogo katika maisha yake.
Alisema kwamba si ajabu inawezekana kipindi hicho ndicho kilisababisha matatizo yote yaliyomkuta. Alisema alikuwa akielekea kubaya.

HATAKI KIJIRUDIE
“Ni kipindi ambacho siwezi kukuhitaji tena katika maisha yangu si kizuri na kinatisha maana kuna wakati nilikuwa sisikii la mtu yeyote hata mama yangu mzazi,” alisema Lulu ambaye baada ya kutoka mahabusu haonekani akirandaranda mjini kama zamani.
Kabla ya utulivu huo alioupata nyuma ya nondo, Lulu alikuwa hakauki kwenye kumbi za usiku za starehe huku akilewa tilalila na kuyaweka maisha yake hatarini endapo angefanyiwa kitu mbaya.
Lulu alihusishwa na kifo cha Kanumba kwa kuwa siku ya tukio alidaiwa kuwa naye eneo la tukio ambapo alikamatwa na baadaye kuachiwa kwa dhamana akisubiri kesi ya kuua bila kukusudia.

SKENDO MPYA
Wakati hayo hayajapoa kumeibuka skendo mpya inayomgusa staa huyo mkubwa Bongo.
Madai mazito yameshushwa na wafuatiliaji wa mambo ya watu kuwa nyuma ya mwanadada huyo anayeng’ara kuna mbunge maarufu anayemiliki jimbo kwa kura za wananchi jijini Dar (tutamtaja baadaye).

ILIKUWA HIVI
Sosi: Hivi ninyi Global siku hizi hamuandiki skendo za mastaa?
Global: Tunaandika sana kwani vipi?
Sosi: Mna habari?
Global: Tunazo nyingi fuatilia magazeti yetu lakini ukitupatia ya kwako tutairusha hewani.
Sosi: Sasa mimi nina habari yangu.
Global: Inakuhusu wewe? Funguka.
Sosi: Hainihusu mimi. Ni ya ‘Kalulu Kadogo’.
Global: Siku hizi amekua, sema Lulu inatosha. Eeh... hiyo habari ikoje?
Sosi: Kwa taarifa yenu siku hizi anatoka na mbunge (anamtaja). Ndiye kamnunulia lile gari analokatiza nalo mjini na kampangishia bonge la mjengo kule Tegeta (Dar). Fuatilieni kwa watu wake wa karibu, naombeni msinitaje.
Global: Hatuwezi kukutaja ngoja tuzame mzigoni.
Gazeti hili lilifanya uchunguzi wake kwa watu wa karibu wa Lulu na kubaini kuwa ni kweli kwa sasa staa huyo amehama Tabata alikokuwa akiishi na mama yake, Lucresia Karugila na kuhamia kwenye bonge la mjengo Tegeta huku akisukuma gari kali (aina haikujulikana mara moja).
Madai mengine yalisema kwamba mke wa mbunge huyo alishamtafuta Lulu na kumuonya kuachana na mume wake.

LULU AFYATUKA
Baada ya kujiridhisha kuwepo madai hayo, juzi gazeti hili lilimtafuta Lulu na kumsomea mashitaka yake mwanzo hadi mwisho ambapo alifyatuka:
“Hivi ni nani anayeleta habari zangu Global? Analipwa na nani? Maana kila kukicha unasikia hili, halijapoa unasikia lingine.
“Si kweli kwamba natembea na huyo mbunge. Kwanza sina mazoea naye. Nakumbuka nilimuona mara moja tu sikumbuki ilikuwa kwenye shughuli gani.
“Huyo mkewe mimi simjui anafananaje. Nasema huko ni kuchafuana kusikokuwa na maana.”

VIPI KUHUSU KUPANGISHIWA NYUMBA?
“Ni kweli nimehamia Tegeta lakini sijapangishiwa, nimepanga mwenyewe. Hivi nikifanya jambo lazima iwe kuna mwanaume? Watu waache hizo. Wabadilike.”

VIPI KUHUSU GARI?
“Gari ninalo muda mrefu nimenunua kwa fedha yangu. Halina mkono wa mbunge, ni jasho langu.”
Kabla ya kuwekwa mahabusu, Lulu aliwahi kudaiwa kuhongwa nyumba na mbunge mwenye kitambi kikubwa, ishu hiyo aliikanusha kwa nguvu zote.
CREDIT-GPL