Sunday, August 18, 2013
Friday, August 9, 2013
MAKAHABA WAENDELEA KUCHAFUA CHUO KIKUU CHA DODOMA[PICHA]
Ongezeko la makahaba mjini Dodoma limeendelea kuwa kero kwa chuo kikuu cha Dodoma na wanafunzi wake kwa ujumla....
Kero hiyo imekuwa ikisababishwa na baadhi ya makahaba hao kujifanya wanafunzi wa chuo hicho kwa lengo la kujiimarisha kibiashara...
Takribani miezi mitatu iliyopita, kahaba mmoja alinasawa na polisi mjini Dodoma akijiuza kwa kujinadi kuwa yeye ni mwanafunzi wa mwaka wa pili chuo kikuu cha Dodoma ..
Baada ya mahojiano ya kina na Polisi Central, ilibainika kuwa kahaba huyo hakuwa Mtanzania na hakuwa mwanafunzi wa chuo chochote hapa nchini na badala yake alikuwa ni raia wa Malawi.
Upekuzi wa polisi ulifanikiwa kunasa ARVs za kupunguza makali ya virusi vya UKIMWI toka kwa mwanamke huyo aliyekuwa akiendesha maisha yake kwa kuuza mwili wake maeneo ya Uhindini mkoani humo.
Mbali na ushahidi huo, mtandao huu umefanikiwa kumnasa binti mwingine anayejiita SECHE MAUTAMU...
Seche ni binti aliyeamua kujiuza kupitia mtandao wa facebook kwa kuwalaghai wanaume kwamba yeye ni mwanafunzi wa UDOM....
Hata katika profile yake, binti huyo ameweka wazi kuwa yeye ni mwanafunzi wa UDOM huku ukurasa wake ukipambwa na picha kadhaa za uchi.....
Kinachotia shaka ni kwamba, picha zote 25 zilizowekwa hazithibitishi moja kwa moja kwamba Seche ni mwanafunzi ama wa UDOM au chuo chochote cha Tanzania...
Picha zilizowekwa ni za gheto lake akiwa UCHI, hali inayotia shaka kubwa ya kukubaliana na uanafunzi wake wa UDOM....
Miongoni mwa wanafunzi tulioongea nao ni wale waliomaliza mwaka 2013, 2012 na 2011. Wanafunzi wote 10 wameshindwa kumtambua Seche na kudai kuwa huyo ni kahaba aliyeamua kuwachafua....
"Huyo siyo mwanafunzi, ni kahaba ambaye ameamua kutuchafua. Kama kweli ni mwanafunzi, mwambieni aweke japo picha moja tu akiwa katika mazingira ya chuo cha UDOM"...Alisema mmoja wa wanafunzi hao.
Kwa kipindi cha mwaka mmoja, mkoa wa Dodoma umekubwa na ongezeko kubwa la MALAYA wanaoishi kwa kuuza miili yao..
Maeneo makubwa yaliyoathiriwa na makahaba hao ni Chako ni chako, Uhindini,eneo la ofisi za hood karibu na club moja ya usiku na maeneo ya ukumbi wa 84.
Cha kushangaza ni kwamba malaya wote hujiita wanafunzi wa UDOM.Wakiulizwa kozi wanazosoma huishia kujiuma na kuwa wakali .
Saturday, August 3, 2013
HARUSI YA MSANII NATASHA KUKUMBUKWA
ILIKUWA ni siku ya kipekee katika historia ya tasnia ya filamu pale mwanadada na mdau mkubwa katika tasnia ya filamu Susan Lewisy ‘Natasha’ alipofunga pingu za maisha na Mr. Alex Humba katika kanisa la Mt. Joseph tarehe 27/7/ 2013 saa sita mchana tofauti na harusi nyingine ambazo zimezoeleka zinazofanyika kila uchwao.
Baada ya harusi hiyo ya kipekee kufungwa na kuhudhuriwa na waheshimiwa mbalimbali wakiwepo wasanii, maharusi walitoka na kuelekea Hotelini kwa ajili ya upigaji wa picha sambamba na kupumzika kabla ya kwenda ukumbini kwa ajili ya kusherekea ukumbi wa kisasa wa Magereza uliopo Ukonga.
Mr & Alex walipendeza kupita maelezo kwani kitu kilichowafanya wapendeze zaidi ilikuwa ni tabasamu lao sambamba na mavazi waliyovaa kwa siku hiyo maalumu kwao na kwa marafiki zao waliofika kwa kumsupport Natasha kama rafiki kipenzi wa jamii nzima ya tasnia ya filamu Swahiliwood, walipendeza sana na kuandika Hitoria ya maisha mapya.
Sherehe hizo zilipambwa na msafara wa mastaa wanaokuja kwa kasi katika tasnia ya filamu Bongo Jalila na Jamira wakiwa na Sonia binti Tyson wakiongozwa na mwigizaji nyota na maarufu asiyechuja Afrika Yvonne Cherryl aka Monalisa ambaye pamoja na umakini alipendeza kweli kweli na kuwa ni pambo la Harusi ya Natasha na kuwaziba midomo wale wote waliokuwa wakikejeli ndoa hiyo.
Uongozi wa FC unatoa pongezi kwa maharusi wetu Mr & Mrs Alex kwa kuungana na kuwa mwili mmoja na si wawili tena, Mungu abariki maisha yao ya ndoa Takatifu iliyofungwa na Mungu. Ameni.
Natasha ni kiungo muhimu sana katika tasnia ya filamu Swahiliwood kwa mawasiliano na mwongozo pia kwa wasanii wote.
Ceo FC Myovela M.
Xclusive Interview: Msikilize Ray C akifunguka kwa mara ya kwanza kuhusu ujio wake mpya
Baada ya kuwa kimya kwa muda mrefu, hitmaker wa Niwe Nawe Milele, Rehema
Chalamila aka Ray C anatarajia kurejea tena kwa kishindo kwenye muziki.
Ray C anatarajia kuonekana rasmi kwenye shughuli za kawaida na za
muziki wiki ijayo. Tumezungumza naye leo kuhusu maisha yake sasa hivi,
alivyobadilika na ujio wake mpya kimuziki.
Kuhusu kama yupo tayari kufanya muziki
I am more than ready, wakati nipo huku nilikuwa naandika andika nina
nyimbo kama tatu nne hivi kali sana. Sema ningependa tu kuwaambia
mashabiki wawe na uvumilivu kwasababu wameniombea sana na wengi kwenye
Instagram, Facebook walikuwa ‘when are you coming back, we miss you’
vitu kama hivyo. Na mimi ningependa kuwaambia tu kwamba wiki ijayo ndio
narudi rasmi, kwa wale ambao walikuwa na wasiwasi, ‘where is Ray C, Ray C
atarudi tena kwenye muziki’ na vitu kama hivyo. Tutaanza kuingia studio
next week, kila kitu kitaanza next week. Lakini kama nyimbo kuandika na
kila kitu vyote viko tayari.
Kuhusu aina ya nyimbo atakazokuwa akiimba zaidi
Nafikiri sasa hivi ntabase kwenye maisha zaidi. Nafikiri watu wanahitaji
kujua mambo ya maisha zaidi. Unajua mimi tangu mwanzo nilikuwa naimba
mapenzi, ofcourse nyimbo za mapenzi zitakuwepo sema ntabase zaidi kwenye
mambo ya maisha.
Kuhusu mabadiliko aliyonayo sasa
Ray C ni kibonge sasa hivi, Ray C amenenepa kidogo. Najua mashabiki
wakiangalia kwenye Instagram wanasema ‘dada vipi bana’ lakini najua
njiani huko ntapunguapungua. Lakini Ray C wa sasa hivi sio kale
kembambaa kale mlikokazoea kale. Sasa hivi Ray C kidogo amevuta shavu
kwahiyo wakiniona wasishangae. Halafu pia kwa sauti niko fit sana. Yaani
all along nilikuwa nafanya zaidi mazoezi kwasababu nimepata sana muda
wa kupumzika, mazoezi ya kuimba, yaani nimeona nipo tofauti na zamani.
Kuhusu sababu za kunenepa
Si unajua tena maisha mazuri, kula kula vizuri, kutulia kwa muda bila
kufanya kazi ndio maana nikafutuka kidogo lakini ntafanya mazoezi,
ntapungua si unajua lazima nipungue kidogo ili niweze kuimiliki
stage,vile nilivyokuwa zamani au better zaidi.
Kuhusu wasanii wapya anaowasikiliza
Namsikiliza sana ambaye namkubali ni mdogo wangu Recho. I think
kwasababu muziki wake kidogo umefanana na wangu kwahiyo napenda ladha
yake halafu kuna Diamond pia namsikiliza, ni msanii ambaye anafanya
vizuri sasa hivi kwahiyo namsikiliza pia kuna kitu gani hapo watu
wanakipendea zaidi niibeibe maideas hapo nifanye kazi nzuri.
Kuhusu alivyojiskia baada ya kusikia nyimbo za Recho
Recho mimi namjua kabla hajatoka na alikuwa anapenda sana nyimbo zangu,
alikuwa anasikiliza sana nyimbo zangu. Mara ya kwanza nimemuona alikuja
akaniambia ‘dada Rehema naomba nikuimbie wimbo mmoja’ akaniimbia
‘Umenikataa Bila Sababu’, akaniimbia nyimbo kama tatu hivi. Kwahiyo
namjua kabla hata hajaingia studio. Kwahiyo nilikuwa najua kabisa
nimemuinfluence kiasi gani.
Tumefurahia kuona maendeleo mazuri ya Ray C na tunamtakia kila lakheri kwenye safari yake mpya ya maisha na muziki.
Msikilize Ray C AKifunguka hapa chini
Subscribe to:
Posts (Atom)